‘Ili mtu aendeshe gari
ya shule, sharti awe na umri usiopungua miaka 35 na sharti awe na umri usiozidi
mika 60, kinyume na hapo ni kosa na adhabu yake ya awali ni faini ya shilingi
laki moja pamoja na kupelekwa mahakamani’
Hii ni kwa mujibu wa
mapendekezo ya sheria ya leseni za usafirishaji SUMATRA sura ya 317 kanuni mpya
namba 421 iliyosainiwa Octoba 6, 2017 na kutangagazwa katika gazeti la serikali
pamoja na kuwekwa katika kanuni za usafirishaji wa magari ya shule.
‘’Kanuni hiyo tayari
imepitishwa, tunasubiri mamlaka husika kupitia idara ya ujenzi, uchukuzi na
mawasiliano watangaze rasmi siku ya kuanza kutumika ambapo itaambatana na elimu
kwa umma kuhusu lengo la mabadiliko haya’’ ameeleza ASP Deus Sokoni,
mwanasheria kikosi cha usalama barabarani nchini.
Aidha, amesema licha ya
sheria kuruhusu miaka 18 kumiliki leseni na kuendesha gari, lakini tahadhari
inachukuliwa baada ya kugundua vijana katika umri mdogo huwa na mihemuko ya
ujana, kwa uendeshaji usiofuata sheria na kanuni za barabarani kwa kuonyesha
mikogo na mbwembwe zinasosababisha ajali.
Hamis Maulid mkuu wa
kitengo cha usafirishaji katika shule ya Alhikma iliyopo Temeke jijini Dar es
salaam anasema umri sio tatizo bali ni umakini wakati wa kuendesha.
‘’Kilichopo kikosi cha
usalama barabarani kitafute jinsi ya kuwadhibiti na kuwaadabisha vijana
wanaogundulika kutofuata sheria, na si kuwazibia riziki za ajira vijana wote’’
Mohamed Juma dereva wa gari za shule Alhikma
No comments:
Post a Comment