Monday, 5 February 2018

Magari ya shule: Dereva kuwa kati ya miaka 35 na 60


‘Ili mtu aendeshe gari ya shule, sharti awe na umri usiopungua miaka 35 na sharti awe na umri usiozidi mika 60, kinyume na hapo ni kosa na adhabu yake ya awali ni faini ya shilingi laki moja pamoja na kupelekwa mahakamani’

Hii ni kwa mujibu wa mapendekezo ya sheria ya leseni za usafirishaji SUMATRA sura ya 317 kanuni mpya namba 421 iliyosainiwa Octoba 6, 2017 na kutangagazwa katika gazeti la serikali pamoja na kuwekwa katika kanuni za usafirishaji wa magari ya shule.

‘’Kanuni hiyo tayari imepitishwa, tunasubiri mamlaka husika kupitia idara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano watangaze rasmi siku ya kuanza kutumika ambapo itaambatana na elimu kwa umma kuhusu lengo la mabadiliko haya’’ ameeleza ASP Deus Sokoni, mwanasheria kikosi cha usalama barabarani nchini.

Aidha, amesema licha ya sheria kuruhusu miaka 18 kumiliki leseni na kuendesha gari, lakini tahadhari inachukuliwa baada ya kugundua vijana katika umri mdogo huwa na mihemuko ya ujana, kwa uendeshaji usiofuata sheria na kanuni za barabarani kwa kuonyesha mikogo na mbwembwe zinasosababisha ajali.

Hamis Maulid mkuu wa kitengo cha usafirishaji katika shule ya Alhikma iliyopo Temeke jijini Dar es salaam anasema umri sio tatizo bali ni umakini wakati wa kuendesha.

‘’Kilichopo kikosi cha usalama barabarani kitafute jinsi ya kuwadhibiti na kuwaadabisha vijana wanaogundulika kutofuata sheria, na si kuwazibia riziki za ajira vijana wote’’ Mohamed Juma dereva wa gari za shule Alhikma

Bunge laombwa kuondoa sheria kandamizi dhidi ya watoto



Wadau wa usalama barabarani wamependekeza kufutwa kwa kifungu cha 39, kifungu kidogo cha 4(b) kinachoeleza kuwa,  watoto wawili kuanzia miaka 3 hadi 12 wanahesabika kuwa abiria mmoja kwenye gari katika sheria mama ya usalama barabarani ya mwaka 1973 (2002).

Akieleza sababu na lengo kuu la marekebisho hayo,  Mwanasheria wa kikosi cha usalama barabarani nchini, Deus Sokoni, ni  kutambua haki za binadamu na ulinzi kwa watoto, kwamba  lazima kila mtoto atambulike kama abiria anayejitegemea bila kujali umri, ili kuongeza ulinzi kwa kutumia vema vizuizi maalum vya kuwalinda watoto wawapo kwenye gari .

‘’Jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa usalama barabarani, shirika la afya duniani (WHO), shirika la afya hapa nchini, SUMATRA, na wizara ya ujenzi tuko katika hatua za kuboresha sheria mama ya usalama barabarani ya mwaka 1973 ili kuondoa changamoto za kisheria, na kilichobaki ni upande wa bunge kupitisha mapendekezo yetu ili watoto kupewa haki yao ya msingi ya kulindwa’’ Deus Sokoni

Wednesday, 15 November 2017

Wanafunzi shule za msingi sasa kufundishwa masomo ya Usalama barabarani



Wanafunzi ni miongoni mwa watumiaji wa barabara. Masomo ya usalama barabarani ni muhimu kwao ili kuwajengea uwezo wa kutumia barabara kwa ufasaha, kufuata sheria, kanuni, na taratibu zote za barabarani.

Tukiachana na wale wanaotumia usafiri wa shule zao binafsi ‘school bus’ idadi kubwa inayobaki hutumia barabara kutembea katika maisha yao ya shule. 

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kutambua umuhimu huo, katika Ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, iliyofanyika Mkoani Kilimajaro wilaya ya Moshi mwezi uliopita, Octoba mwaka huu 2017, aliagiza shule zote za msingi nchini kutoa elimu ya usalama barabarani kama yanavyofundishwa masomo mengine.

Lengo kuu la mafunzo hayo, ni kuwajengea uwezo wananfunzi wa shule za msingi kutambua umuhimu wa Usalama barabarani wangali wadogo ili kuwaepusha na ajali zitokanazo na kutotambua matumizi sahihi ya alama za barabarani pindi wanapotumia barabara.

Vile vile ili kuzitambua sababu sababishi za ajali na madhara yake, ambazo ni Mwendokasi, ulevi, kutofunga mikanda na vizuizi vya watoto kwenye magari 'Child restraints', pamoja na kutovaa kofia ngumu kwa waendesha pikipiki.

Magari ya shule: Dereva kuwa kati ya miaka 35 na 60

‘Ili mtu aendeshe gari ya shule, sharti awe na umri usiopungua miaka 35 na sharti awe na umri usiozidi mika 60, kinyume na hapo ni ...