Wanafunzi ni miongoni mwa
watumiaji wa barabara. Masomo ya usalama barabarani ni muhimu kwao ili
kuwajengea uwezo wa kutumia barabara kwa ufasaha, kufuata sheria, kanuni, na
taratibu zote za barabarani.
Tukiachana na wale wanaotumia
usafiri wa shule zao binafsi ‘school bus’ idadi kubwa inayobaki hutumia
barabara kutembea katika maisha yao ya shule.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kutambua umuhimu huo, katika Ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani, iliyofanyika Mkoani Kilimajaro wilaya ya Moshi mwezi uliopita,
Octoba mwaka huu 2017, aliagiza shule zote za msingi nchini kutoa elimu ya usalama
barabarani kama yanavyofundishwa masomo mengine.
Lengo kuu la mafunzo hayo, ni
kuwajengea uwezo wananfunzi wa shule za msingi kutambua umuhimu wa Usalama
barabarani wangali wadogo ili kuwaepusha na ajali zitokanazo na kutotambua
matumizi sahihi ya alama za barabarani pindi wanapotumia barabara.
Vile vile ili kuzitambua sababu sababishi za ajali na madhara yake, ambazo ni Mwendokasi, ulevi, kutofunga mikanda na vizuizi vya watoto kwenye magari 'Child restraints', pamoja na kutovaa kofia ngumu kwa waendesha pikipiki.
No comments:
Post a Comment